Jihusishe
Disciple Nations Alliance ni mtandao wa waumini
unaopanuka duniani kote. Tazama jinsi unavyoweza kujihusisha!
Jiunganishe
Jiandikishe kwenye jarida letu, na ufuatilie DNA kwenye Faceboook na Istragram. Pia, jiunge na Kingdomizer Network, au ukipenda, mtandao wa waeneza Ufalme wa Mungu!
Jifunze
Anza safari yako na Coram Deo, kozi zetu za mtandaoni zimeundwa kwa matumizi ya watu binafsi, makanisa, na mashirika.
Toa
Mojawapo ya njia bora zaidi unayoweza kusaidia kazi ya Disciple Nations Alliance ni kupitia zawadi ya kifedha.
Jiunge na Mtandao wa Kingdomizer
Mueneza Ufalme wa Mungu (Kingdomizer) hueneza ukweli, wema, na uzuri wa Ufalme wa Mungu ulimwenguni ambapo anaishi. Mtandao huu ni wa wale ambao wameguswa sana na mafundisho ya DNA. Watu hawa wanataka kuendelea kukua kwa kina katika uelewa wao na kujiungana na watu wengine wa kueneza Ufalme wenye mawazo sawa duniani kote ili kujifunza pamoja, kubuni, kupanga mikakati, kuunganisha, na kuwaongoza mataifa kwa ufanisi zaidi.
Kwa nini ujiunge na Mtandao wa Kingdomizer?
Mafunzo
Pata taarifa za mapema na ufikiaji wa fursa ya mafunzo maalum yanayotolewa na wafanyakazi wa DNA na wakufunzi wa kimataifa.
Rasilimali
Pata punguzo na ufikiaji wa mapema wa vitabu, mafunzo na vifaa vya kufundisha.
Matukio
Pokea mialiko na jiunge na waeneza Ufalme wa Mungu kutoka ulimwenguni kote kwa ajili ya mikutano ya kikanda na kimataifa.
Mawasiliano
Pata taarifa maalum kutoka DNA na usikie shuhuda za kutia moyo kutoka kwa waeneza Ufalme wa Mungu wengine.
Kujiunganisha
Jiunge na waeneza Ufalme wa Mungu wengine wenye mawazo yanayofanana ulimwenguni kote ili kujifunza pamoja, kupanga mikakati,na kuwafundisha mataifa kwa ufanisi zaidi.
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara
Mtandao wa Kingdomizer ni wa wale ambao wameguswa kwa kina kutokana na mafundisho ya DNA na wangependa kuendeleza wito wao wa Ufalme. Hii inamaanisha kuwa umeshashiriki na maudhui ya mafundisho ya DNA kupitia kitabu, au mafunzo ya mtandaoni, au mfululizo wa programu ya sauti ya mtandaoni, au mfululizo wa video. Zaidi ya hayo, umeisha guswa kwa namna ambayo unataka kuendelea kuelewa zaidi na kuishi kwa mtazamo wa kibiblia na wito wako wa Ufalme.
Kama mueneza Ufalme wa Mungu, unaweza kutarajia kuendelea kupokea matangazo ya jumla kutoka kwa DNA, rasilimali na habari na zaidi ya hayo, utapokea taarifa maalum za mara kwa mara kwa fursa mpya za mafunzo, uzinduzi wa vitabu na punguzo, na mialiko ya matukio.
Hakuna gharama ya kujiunga na huu mtandao isipokuwa kujitolea na shauku ya kukua katika wito wako wa Ufalme.
Kujiunga ni rahisi.
Mtandao huu ni wa bure kabisa na umepangwa kuwawezesha na kuunganisha waeneza Ufalme wa Mungu ulimwenguni.
- Jaza fomu
- Kuwa mweneza Ufalme wa Mungu
Je, wewe ni mzungumzaji wa lugha nyingi? Jisajili kwenye Kingdomizer Network kwa Kiingereza, Kihispania, Kireno, Kifaransa, au Kiarabu ili kupokea taarifa zote mpya!